Bendera ya Tanzania imetangazika tena hivi karibuni katika mchezo wa riadha nchini Korea Kusini. Kutangazika huko kumefanywa na mwanaridha Alphonce Simbu ambaye ameibuka kidedea kwa kushinda mbio za barabarani au maarufu kama Marathon ambazo zimefanyika hivi karibuni katika jiji la Daegu. Aliibuka mshindi wa medali ya fedha katika mashindano ya Daegu International Marathon. Ameshinda medali hiyo kwa kukimbia umbali wa kilomita 42 kwa kutumia masaa 2 dakika 7 na sekunde 55. Hakika kwa kufanya hivyo alilitangaza taifa na halikadhalika aliendeleza rekodi yake nzuri katika mbio ndefu za barabarani (Marathon). Amekuwa ni mwanamichezo ambaye ana nidhamu ya hali ya juu na hakika hali hiyo imemsaidia sana katika kufanya vizuri katika mashindano ya kimataifa.
Nyota yake ilianza kuchomoza katika mashindano ya kimataifa katika olimpiki za majira ya baridi ambazo zilifanyika mwaka 2016 aliposhiriki mbio ndefu na kushika nafasi ya tano. Baada ya hapo akashinda mbio za mara ya 14 za Mumbai Marathon ambazo zilifanyika mnamo mwezi januari mwaka 2017. Akasonga mbele na kushika nafasi ya 16 katika mashindano ya riadha ya dunia ya marathon kwa upande wa wanaume ambayo yalifanyika katika mji wa Doha ambao upo katika nchi ya Qatar na hiyo ilikuwa mnamo mwaka 2019. Mnamo mwaka uliofuatia alishika nafasi ya 7 katika mbio ambazo zilifanyika mashindano ya Olimpiki ya msimu wa baridi ambayo mnamo mwaka 2020.
Mwaka uliofuatia alishinda medali ya shaba ambayo aliipata katika mbio za jumuiya ya madola ambazo katika kipengele cha wanaume. Kwa ujumla amewahi kushinda medali ya fedha katika mbio za kidunia. Amewahi kuingia mara mbili katika 8 bora kwenye mbio za olimpiki ana medali moja ya shaba katika mbio za jumuiya ya medali, ameingia mara moja katika nane bora ya mashindano ya All African games, amewahi kuwa bingwa mara moja wa mashindano ya kitaifa. Hakika wasifu wake umejaa ushindi ambao amekuwa anaupata mara kwa mara kwenye mashindano mbalimbali ya mbio duniani.
Simbu anaingia moja kwa moja kwenye orodha ya magwiji wa michezo nchini Tanzania na anatakiwa ajitunze vizuri Zaidi afya yake ya kimwili na kiakili ili azidi kupambana na kuweza kupata medali nyingi Zaidi. Bado anapambana na anaonyesha kwamba anaweza kushinda mataji mengi Zaidi. Simbu bado ana nafasi ya kuja kuvunja rekodi zilizowekwa na wanariadha nguli wa nchi ya Tanzania kama vile Juma Ikang’aa Filbert Bayi na wengineo.
Simbu kama ataendelea na nidhamu aliyonayo kimichezo itamikisha mbali Zaidi. Menejimenti inayomsimamia Simbu kwa sasa inatakiwa ihakikishe Simbu anapata matangazo ya biashara kwani ana kila sifa ya kumwezesha kupata matangazo ya kibiashara. Wanatakiwa wampatie pia matangazo ambayo yatamuongezea kipato chake. Menejimenti yake inatakiwa ihakikishe kuwa anapata mazoezi ya kutosha ya kumwandaa aweze kushiriki mashindano ya kimataia na afanye vizuri na pia awe anakula milo ambayo itamsaidia kujiandaa vizuri katika mashindano hayo.
Serikali kwa upande wake imempatia tuzo za uanamichezo bora ambazo alizipata mwaka jana katika hafla ya tuzo za wanamichezo ambazo ziliandaliwa na baraza la michezo Tanzania (BMT) ambazo zilifanyika ukumbi wa mikutano wa Mlimani City jijini Dar es salaam. Kwa kuwa mwanariadha huyo amefanya vizuri katika mashindano mbalimbali basi haina budi hata shule mojawapo ya umma ibadilishwe jina na kasha ipewe jina lake kama sehemu ya kumkumbuka makubwa aliyoyafanya kwenye riadha.