Menu
in , , ,

AFCON2015: Senegal, Ghana, Algeria kitendawili


*Bafana Bafana wabaki mkiani

Kundi C limedhihirisha kwamba ni la ‘kifo’ kutokana na mwelekeo wa matokeo, ambapo baada ya mechi mbili mbili mambo bado ni magumu.
Senegal japokuwa wanaongoza, wana kazi ngumu wanapokutana na Algeria wiki ijayo, wakati Waarabu hao na Ghana wanapigania nafasi mbili za kuvuka kadhalika.
Kwenye mechi za Ijumaa, Senegal walioanza kwa kuwafunga Ghana, walitoka nyuma na kwenda sare ya 1-1 na Afrika Kusini na sasa wanaongoza kwenye kundi lao.

Ilichukua sekunde 62 tu za kipindi cha pili kwa Oupa Manyisa wa Afrika Kusini – Bafana Bafana kufungua kitabu cha mabao, Senegal wakajitahidi kutafuta la kusawazisha na Sadio Mane akalipata lakini likakataliwa kwa madai aliotea lakini Kara Mbodji akaswazisha.

Simba wa Teranga bado hawajavuka hatua ya makundi, lakini wamesababishia matatizo Afrika Kusini ambao kwa kuwaweka mkiani, wakiwa na pointi moja na hivyo hawataweza kuvuka.
Katika mechi ya awali, Ghana walifanikiwa kuwafunga Algeria 1-0, ambapo walicheza dakika 89 bila kupata mshindi, na wakati ikidhaniwa mambo yangeisha kwa suluhu, nahodha Asamoah Gyan aliyekuwa anaumwa malaria akafunga katika dakika ya 90.

Kwenye mechi hiyo ya Ijumaa kulikuwa na nafasi chache sana za kufunga Algeria wenyewe walikosa nafasi pekee ya wazi wakati Nabil Bentaleb alipobetua mpira kutoka umbali wa yadi 12 katika dakika ya 20 lakini hakufanikiwa kufunga.

Gyan aliikosa mechi ya kwanza dhidi ya Senegal kutokana na maradhi yaliyokuwa yakimkabili, lakini alionesha ukali aliporejea uwanjani. Senegal waliwafunga Ghana na wanaweza kuvuka iwapo watakwenda sare na Algeria Jumanne ijayo. Afrika Kusini wakiwafunga Ghana, basi Sengal watavuka pia.

Ghana na Algeria wamefungana kwa pointi tatu wakati Senegal wanaongoza wakiwa nazo nne na Afrika Kusini wanayo moja. Ghana wangependa kuona Senegal wakiwafunga au kwenda sare na Algeria ili wao wawe na kazi moja tu kuwafunga Afrika Kusini na kuwazidi pointi Algeria na kusonga mbele.
Leo Ivory Coast wanacheza na Mali wakati Cameroon wanakipiga na Guinea Bissau.

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Leave a Reply

Exit mobile version