Menu
in

PSPF yatoa msaada wa vitanda Temeke Hosp

MFUKO wa Pensheni wa PSPF, imeisaidia hospitali ya wilaya ya Temeke, vitanda, magodoro na mashuka ili kusaidia serikali katika juhudi zake za kupunguza uhaba wa vifaa vya hospitali za uma.

Msaada huo ambao ni utekelezaji wa maombi ya Mbunge wa viti maalum, Angela Kairuki, alioutoa kwa uongozi wa PSPF, baada ya kutembelea hospitali hiyo wakati akiwa naibu waziri wa Sheria na Katiba, na kukuta akina mama wajawazito waliofika hospitalini hapo kujifungua wengine wakilala chini kutokana na uhaba wa viotanda, alisema Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Abdul Njaidi na kuongeza PSPF, kwa kuwa ni Mfuko unaotoa huduma kwa jamii, nao hauna budi kutoa sehemu ya faida na kuirejesha kwa jamii kwani wengi wao wanaofika hapo hospitali kwa ajili ya matibabu ni wanachama wa Mfuko na wengine ni wanachama watarajiwa wa Mfuko.

Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Bw. Abdul Njaidi, (wa kwanza kulia), akiungana na Mbunge wa viti maalum, Angela Kairuki, (wa pili kulia), mkurugenzi wa manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam, Photidus Kagimbo, watatu kulia), mganga mfawidhi wa hospitali ya Temeke, Dkt. Amani Malima, (wane kulia) na Mganga Mkuu wa Manispaa ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, (wakwanza kushoto), wakati PSPF, ikikabidhi msaada wa vitanda, mashuka na magodoro kwa hospitali hiyo, Desemba 7, 2015. Msaada huo ni utekelezaji wa ahadi ya Mfuko baada ya kuombwa na Mh. Angela Kairuki.

Kufuatia maombi hayo Mfuko huo umekabidhi vifaa hivyo leo Desemba 7, 2015, ambapo Afisa Uhusiano Mwandamizi wa Mfuko huo Bw. Abdul Njaidi, alikabidhi vifaa hivyo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu.

Akipokea vifaa hivyo katika hafla iliyohudhuriwa na Mkurugenzi wa Mnaispaa ya Temeke, Photidus Kagimba, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Dkt. Sylvia Mamkwe, na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Temeke, Dkt. Amani Malima, aliishukuru PSPF, kwa moyo huo wa kusaidia jamii.

Maafisa wa hospitali ya Temeke wakijiandaa kupokea msaada wa vitanda toka kwa afisa wa PSPF, Bw Njaidi.

“PSPF mmeonyesha moyo wa uungwana kwa kusaidia akina mama zetu wakati wakisubiri kupatiwa huduma wakati wa kujifungua basi wawe na mahala pazuri pa kulala.” Alisema

Written by Israel Saria

For the last 20 years I have been working as a football pundit. This experience has provided me with a very useful insight into football and the opportunity to carry out extensive research into the game including its players, the stadiums, the rules and tactics and I have also been grateful to meet a wide range of people connected to football in the UK, Tanzania, Germany .....

Exit mobile version